Monday, 26 August 2013

MTOTO WA MIAKA 8 AOLEWA NA MWANAUME WA MIAKA 38...POLISI WAINGILIA KATI.



Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samson (38), mkazi wa Kijiji cha Mindukeni, Tarafa ya Tarawanda katika Wilaya ya Bagamoyo, Pwani amefanya maajabu ya milenia baada ya kudaiwa kuoa mtoto mwenye umri wa miaka nane .

Habari za kiuchunguzi zilisema kuwa mwanaume huyo ambaye tayari alishaoa mke wa kwanza, alidaiwa kumtorosha mtoto huyo nyumbani kwao, Iringa.


Ilidaiwa kuwa Samson alifanya tukio hilo kwa kushirikiana na mjomba wa mtoto huyo, wakati akichunga mbuzi mkoani Iringa.

Habari zilieleza kuwa baada ya Samson kumtorosha mtoto huyo kijijini kwao alimpeleka kijijini Mindukeni, Pwani na kumuweka kinyumba akiwa ni mke wake wa pili.


Ilidaiwa kwa kuwa mtoto huyo analingana na watoto wake kwa mke wa kwanza, alimweka chumba kimoja na wanaye.

Kabla ya ishu kubumburuka, Samson alikuwa akiishi na mtoto huyo akiwa ni mke mdogo huku akimtumia kufanya kazi mbalimbali kama kuchunga mbuzi, kuchota maji kisimani na kusaidia kubeba au kulea watoto wa mke mkubwa.
 
Kwa mujibu wa mtoto huyo, hadi sasa hajui alifikaje kijijini hapo na wala hatambui jinsi ya kurudi kwao kwani walimuiba tu.

Alisema baada ya kufikishwa kijijini hapo, alikuwa akilala chumba cha watoto na mwanaume huyo akitaka kumuingilia anaingia chumbani humo na kufanya naye mapenzi kisha kurudi kwa mke mkubwa.
 

“Nilikuwa naumia wakati akiniingilia, alikuwa anakuja chumba tunacholala na watoto wake wengine, ananichukua pembeni na kufanya mapenzi, akimaliza anarudi kwa mke mkubwa,” alisema mtoto huyo na kuongeza:
 

“Kusema kweli mwanzoni nilikuwa nasikia maumivu makali hadi nilipokuja kuona ni kitu cha kawaida.”

Mtoto huyo alisema kuwa kila kulipokucha alikuwa anaona aibu kwani wale watoto wengine wanalingana naye hivyo alikuwa akiumia kufanyiwa kitendo kama hicho cha ukatili na mtu ambaye ni sawa na baba yake.


Aliendelea kusema kuwa aliumia kupelekwa katika kijiji hicho na kuishi na mwanaume huyo na tayari ameshakaa miaka minne kama mke wake, akimuingilia mara kwa mara na kumsababishia maumivu.  


“Nimeishi naye muda mrefu kama miaka minne, natamani kurudi kwetu nikasome,” alisema mtoto huyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!