Thursday, 1 August 2013

MTOTO WA MIAKA 6 ANAJISIWA, AUAWA KWA KUKATWA SHINGO NA MIKONO


MTOTO wa miaka sita amenajisiwa na kisha kuuawa kikatili kwa kukatwa shingo na mkono kwa panga na kijana mwenye umri wa miaka 14 kinyama kuwa Narbeth Haule anayedaiwa kuwa mkulima na mkazi wa kijiji cha Ijoka hali inayodhihirisha alitenda unyama huo pasipokujali udugu wa kuheshimiana na kusaidiana katika mambo mbalimbali ambao wamekuwa nao wakazi wa vijiji vya wilayani Rungwe na mkoa wa Mbeya kwa ujumla.

Kamanda Athuman alisema awali baada ya kubakwa mtoto Janeth aliapa kwenda kuwaambia wazazi wake akiwemo baba yake juu ya unyama aliotendewa na ndipo kijana huyo aliamua kwenda nyumbani kwao kuchukua upanga na kuja kumkata mtoto huyo shingoni na mkono wake wa kulia lengo likiwa ni kupoteza ushahidi wa kubaka.

Alisema tayari jeshi hilo linamshikilia kijana huyo na kuwa taratibu mbalimbali za kisheria zinaandaliwa ili aweze kufikishwa mahakamani na mkono wa sheria kuchukua mkondo wake kwa roho ya ukatili na unyama aliyo nayo dhidi ya binadamu wenzake.

MBEYA YETU.
 






 



 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!