Sunday, 4 August 2013

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA JERRY SILAA ATEMBELEA KLINIKI YA KUSAIDIA WALEMAVU WA KUSIKIA.


 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahia jambo alipokuwa akimskiliza kutoka kwa Mkurugenzi wa Montage Bi Teddy Mapunda mara baada ya kuwasili katika eneo  ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya vifaa vya kusaidia usikivu jana jijini Dar es Salaam.Huduma hii ya kijamii ya kusiadia watu wenye matatizo ya kusikia imekuwa ukitolewa kwa ushirikiano wa taasisi za Starkey ya Marekani, Montage ya Tanzania na Serena Hotel ambapo hii ni mara ya tatu tokea wameanza kutoa huduma hiyo.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuwekea kifaa cha kusaidia usikivu mwanafunzi aliyetambulika kwa jina moja la Adrian ambaye jana jijini Dar es Salaam.Huduma hii ya kijamii ya kusiadia watu wenye matatizo ya kusikia imekuwa ukitolewa kwa ushirikiano wa taasisi za Starkey ya Marekani, Montage ya Tanzania na Serena Hotel ambapo hii ni mara ya tatu tokea wameanza kutoa huduma hiyo. 
 Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akiwa na mwanzilishi ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya usikivu William Austin alipotenmbelea kliniki ya kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya usikivu hapa nchini iliyoratibiwa na Taasisi ya kusaidia usikivu (Starkey) kwa kushirikiana na kampuni ya Montage ya Tanzania na Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
 Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akimpa mazoezi ya kusikia mmoja wa wagonjwa  alipotenmbele eneo ilipokuwa inatumika kwa ajili ya kliniki ya kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya uskivu hapa nchini iliyoratibiwa na Taasisi ya kusaidia usikivu (Starkey) kwa kushirikiana na kampuni ya Montage ya Tanzania na Serena Hotel
 Mwanzilishi wa StarKey taasisi ya kusaidia usikivu ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya usikivu William Austin mwenye fulana ya bluu akifuatilia maendeleo ya mgonjwa wa usikivu wakati akipewa mazoezi nkufuatia kupatiwa kifaa cha kumsaidia kusikia  jijini Dar es Salaam..
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa pili kushoto katika picha ya pamoja na waratibu wa kliniki ya kuhudumia watu wenye matatizo ya kutosikia alipotembelea kliniki hiyo  jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Starkey Judith Robert, Mkurugenzi wa Montage Teddy Mapunda na Mkurugenzi wa Masoko wa Serena Hotel Serafin Lusal

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!