Sunday, 4 August 2013

KIJANA HAMIS MOHAMED AIPATIA SIFA TANZANIA HUKO MAREKANI, RAIS KIKWETE AMPONGEZA, NI YATIMA AMBAYE AWALI ALILELEWA KATIKA KITUO CHA YATIMA CHA DOGODOGO CENTER DSM.

Rais Jakaya  Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa  kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye  awali
alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo  Dar es Salaam,
alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika
Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre

 Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 
 Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani
 Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
 Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
 Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!