Tuesday, 27 August 2013

MALI ZA VIGOGO WAUZA "UNGA" ZAKAMATWA, MAJINA 111 YA MAPAPA AU MAPUNDA YATAJWA BADO MANYANGUMI


VIGOGO 111 wanaosadikiwa kujihusisha na biashara yharamu ya madawa ya kulevya nchini wameanza kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kukamata mali zao, Uwazi lina mpango mzima.
Kwa mujibu wa vyanzo makini ndani ya jeshi hilo, pia vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo  walikamatwa na kiasi kikubwa cha ‘unga’ ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita.
Kuhusu mali ambazo ni magari, ilidaiwa kuwa kufuatia taarifa zilizowataja wauza unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia magari hayo na kufanya uchunguzi wa uhalali wake.
“Kuna watu walitajwa majina, wakafuatiliwa, magari yao yakakamatwa na kufanyiwa uchunguzi, lakini cha kushangaza baadhi yao  wameingia mitini na kutelekeza magari yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kilisema baadhi ya magari hayo ni Mercedes Benz, Jeep, Toyota Spacio, Toyota Galsira, Toyota Mark II, Nissan Patrol 4x4 GL, Toyota Land Cruiser na Toyota Prado.   
Uwazi lilifanikiwa kunasa majina ya vigogo waliokamatwa wakiwa na unga  na kiasi walichokamatwa nacho.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mahakama mbalimbali nchini na ndani ya jeshi la polisi umebaini kuwa, kesi za watuhumiwa hao zinaendelea kuunguruma kortini  japokuwa kasi yake si ya kuridhisha.

POLISI WABUNI MBINU MPYA
Vyanzo hivyo viliendelea kudai kwamba polisi wamebuni mbinu mpya ya kuwakamata vigogo wa madawa ya kulevya wakiamini itawapa mafanikio zaidi.
“Siku hizi si kama zamani, jeshi la polisi tumebuni mbinu mpya ya kuwakamata hawa jamaa (vigogo). Mbinu hii italeta mafanikio makubwa zaidi,” alisema mtoa habari wetu.

WAPAMBANAJI WA UNGA HATARINI
Taarifa zaidi zinadai kwamba usalama wa viongozi wanaopambana na wahusika wa unga nchini upo shakani kutokana na vitisho vinavyotolewa na mtandao huo duniani kote.
Inaaminika kuwa wengi wanaopambana au kupiga vita madawa ya kulevya, hususan viongozi na waandishi wa habari, hutendwa vibaya wakati mwingine kuuawa kabisa.

UWAZI LAMSAKA KAMANDA NZOWA
Kufuatia taarifa hizo za kiuchunguzi, katikati ya wiki iliyopita, mapaparazi wetu walimtafuta Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu zoezi zima la kamatakamata ya wanamtandao hao.
Kamanda Nzowa alisema zoezi la kuwakamata wanaojihusisha na biashara hiyo linaendelea vizuri.
Alisema mpaka Mei, mwaka huu kikosi chake kimeshakamata kiasi kikubwa cha unga na kuongeza kuwa anaamini kasi ya biashara hiyo nchini imepungua sana.
Aliongeza kuwa askari wake wamejipanga vizuri na wana mafunzo maalum ya kuwatambua watu hao hatari.

VIGOGO HUWALISHA KIAPO KIBAYA  WANAOWABEBESHA
“Tumewakamata ‘mapapa’ (wauza unga wadogo) wengi sana na tunahakikisha kwamba ‘nyangumi’ (wauza unga vigogo)  nao hawachomoki.
“Mara nyingi vigogo wamekuwa wakiwalisha kiapo kibaya vijana wanaowabebesha unga kwamba  ikitokea wakakamatwa wasiwataje lakini nao tunawabana kitaalam mpaka wanawataja, kwa sasa bado tunaendelea kuwadaka,” alisema Kamanda Nzowa.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lake dhidi ya wauza madawa ili kutokomeza kabisa biashara hiyo.

ULINZI VIWANJA VYA NDEGE NCHINI SASA NI MOTO
Katika maongezi yake, Afande Nzowa alisema ulinzi umeimarishwa katika viwanja vya ndege, bandarini, mipaka ya nchi na sehemu zote zinazohisiwa kuweza kupitishwa madawa hayo.

AANIKA MAJINA 111 
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kuweka wazi takwimu ya ukamataji wa watuhumiwa hao kutoka mwaka 2009 hadi Mei, 2013.
Orodha chini inabainisha kiasi na aina ya madawa waliyokamatwa nayo katika mabano.
Steven  Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroin gram 1,800), Khatibu Bakari Khatibu, Khalid Salim Maunga, (cocaine gramu 1,007.4), Dhoulkefly  Awadh, (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua Kipevu (heroin gramu 31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000), huyu alikamatwa akiwa na Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!