Tuesday, 27 August 2013

GURUMO: NIMESTAAFU MUZIKI SINA HATA BAISKELI"

Gurumo: Nimestaafu muziki sina hata baiskeli
Gwiji wa muziki wa dansi nchini, Muhidini Gurumo (73) ametangaza rasmi kuacha kujishughulisha na muziki baada ya kuitumikia fani hiyo takribani miaka 53.

Gurumo alitangaza kustaafu muziki huo jijini Dar es Salaam jana wakati alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema ameamua kuachana na muziki huo kutokana na umri kumtupa mkono pamoja na maradhi ya mara kwa mara, lakini licha ya hivyo bado ataendelea kutoa ushauri wa muziki katika bendi yake ya Msondo Ngoma na kwa wanamuziki wengine nchini watakaohitaji ushauri kutoka kwake.

“Leo nimekuja kuwaaga rasmi wanamuziki na mashabiki wangu kwa ujumla, na nimeamua kustaafu kwa moyo mmoja, pia kustaafu kwangu hakuzuii kutoa ushauri katika bendi ya Msondo na kwa wanamuziki wala kufundisha wapiga ala kwani nina kipaji cha kumfundisha mpigaji wa chombo chochote kwa kutumia mdomo wangu,” alisema Gurumo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!