Polisi nchini Kenya
wanachunguza kisa ambacho kichwa cha mtu aliyeuawa kilipatikana kimewekwa nje ya
afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini
Nairobi. Kifurushi hichi
kilichokuwa kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono
miwli ya binadamy iliyojaa damu.
kando
ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye
utakayefuata''.
Tangu uteuzi wake, kamishna
huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia marekebisho idara ya polisi ambayo
inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa idara ya
polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na tukio hilo na kuwa bado
wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika miezi ya hivi
karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo inayoongozwa na Kavuludi na ofisi
ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha
idara hiyo.
Chanzo - BBC
Swahili
No comments:
Post a Comment