Msanii Diamod afunguka mengi juu ya historia ya maisha yake, na changamoto alizozipitia katika safari yake ya mziki mpaka kufikia hapa, katika semina ya Fursa, inayoandaliwa na Clouds Fm katika kila mkoa tamasha la Fiesta linapopita.
Kupitia semina ya fursa mkoani Tabora, Diamond alikua ni mmoja wa wasemaji/watoa mada mbele ya mamia ya maraia wa tabora katika kuhamasisha vijana kuzijua fursa na kuzitumia ili kujiletea maendeleo.
Ndani ya dakika tisa alizoongea Diamond ameongea mengi ikiwemo, kipindi cha mwaka 2008/09 ambapo alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichopo Mikocheni, na kupewa ujira wa sh 2000 kwa masaa 8, huku nauli ikimgharimu sh 1000 mpaka kufika kwao na hapo chakula ni zaidi ya 1000 so hakua na hela yoyote ya ku-save
No comments:
Post a Comment