Friday 26 July 2013

SAKATA LA BI DADA ALIYETIMULIWA KANIKASINI AKIWA NA VAZI LA NUSU UCHI ADAI KUWA KANISA LIMEMUONEA, WALIMSUKUMA AKAANGUKA NA WAMEHARIBU VIATU VYAKE VYA "UINGEREZA"..!!!


 
Wakati mwanamke wa kivazi kilichositisha ndoa kanisani kwa dakika kadhaa akidai hakuwa na tatizo kuvaa vile, Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Peter, Yohane Maboko, amesisitiza kuwa alikiuka maadili ya Kanisa.

Mwanamke huyo ambaye ameendelea kukataa kutaja jina lake, huku njia zingine zikimtaja kwa jina la Restituta Kalemera, alidai juzi kuwa kivazi hicho cha mabega wazi hakikuwa tatizo kanisani, bali ni unyanyasaji tu wa Katekista huyo.
Akizungumza  juzi, alidai kuwa Katekista Maboko alimsukuma na kumwangusha katika ngazi ndefu za Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.

"Wakati Katekista akinitaka nitoke nje, ghafla alinisukuma nikaanguka kwenye ngazi na kudakwa na mtu mwingine aliyeniokoa, la sivyo ningeumia vibaya," alidai.

Alidai kilichomsikitisha ni kudaiwa kutaka kuingia kanisani akiwa amevaa nguo zilizoacha mwili wazi, jambo ambalo si la kweli, kwa kuwa alikwenda kanisani hapo akiwa na kitambaa kilichofunika mwili.

"Nilipofika kanisani, nilikutana na Katekista akimrudisha mtu mwingine, ghafla alitokea bibi harusi aliyevalia nguo ambazo hazikuruhusiwa kanisani, akaniomba skafu niliyokuwa nayo, nikampa nami kubaki wazi mabegani,"
alidai.



 Aliendelea kudai, kuwa Katekista alipomsukuma na kuanguka, baada ya kudakwa alichanganyikiwa akidhani kanisani ni sehemu ya malumbano, akakimbilia ndani kutafakari, huku kiatu chake alichonunua nje ya nchi (Uingereza) kikiwa kimeharibika.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!