Friday 26 July 2013

FAHAMU HISTORIA YA MJI WA ARUSHA.

 

 

 

 

Arusha ni mji ulio kaskazini mwa Tanzania. Mji huu umezungukwa na baadhi ya manzara maarufu barani Afrika pamoja na mbuga za wanyama. Mji upo kando ya Mlima Meru kwenye ncha ya mashariki mwa Bonde la Ufa. Hali ya hewa ni nzuri sana. Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Tarangire na mlima Kilimanjaro zipo karibu na mji huu. Mjı huu ni makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Idadi ya wakazi wa mji huu kulingana na sensa ya 2002 ni 1,288,088. Kuanzia 1994 mjı huu umekuwa makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda






Jiografia na hali ya hewa

Licha ya kuwa karibu na ikweta mwinuko wa Arusha wa mita 1400 kusini mwa Mlima Meru hufanya hali ya hewa yenye ubaridi na unyevu mwingi. Viwango vya joto ni kati ya daraja 13 na 30 na daraja 25 kwa wastani. ina nyakati tofauti za mvua na ukame na huwa inakumbwa na upepo wa msimu unaovuma toka Bahari Hindi. Dini ya wakazi wa Arusha ni wakatholiki, waanglikani, Wayahudi, Waislamu, na Wahindu.

 

Historia ya kisasa

Hati rasmi za uhuru wa tanzania zilitiwa sahihi hapa na Uingereza mwaka 1961. Azimio la Arusha la kujitgemea lilipitshwa mjini hapa karibu na maeneo ya mnara wa saa.

Makubaliano ya Arusha accords ya kusitisha vita nchini Rwanda yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993.

Viwanda na Uchumi

Sekta ya msingi ya Mkoa wa Arusha ni kilimo, wazalishaji wa maua na mboga hutuma mazao yao ya hali ya juu Ulaya. Wakulima wadogo wadogo wa kahawa waliathiriwa vibaya na mgogoro wa kahawa wa miaka ya karibuni. Arusha ina viwanda kadhaa kwa mfano viwanda vya tairi, mimea na madawa.

Mkoa wa Arusha ni chanzo pekee cha madini ya Tanzanite duniani, madini haya yanazalishwa kwa wingi sana na makampuni ya madini.

Utalii pia ni unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Arusha. Utalii unachukua nafasi ya pili kwa mchango wa mapato Tanzania. Kutokana na eneo la mji kuwa karibu na vivutio maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro, Serengeti, na Ngorongoro, Arusha imekuwa maarufu kwa watalii wanaotembelea Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii.

Arusha ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na pia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda na Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu.

 

Wilaya

Bishop's Cathedral of Arusha.

Arusha Clock Tower.

Miongoni mwa maeneo maarufu ya Arusha ni Eneo la biashara, Sekei ambayo ipo Kaskazini-Magharibi, Njiro, kitongoji kinachokua haraka Kusini mwa mji naSoko la Tengeru.

Kaskazini mwa Arusha ni Wilaya ya Karatu, Ngorongoro, Monduli, Arumeru na Longido ambayo ipo kando ya barabara ya Arusha-Nairobi na ni zaidi ya dakika 90 kaskazini mwa Arusha kwa daladala. kambi ya Safari ya Robanda iko nje tu ya mbuga Serengeti. Kuna idadi kubwa ya wanyama kwa mfano Nyumbu na Zebra, tembo na twiga. Aina ya wanyama wengine ni pamoja na simba, fisi, Swala, topi, nyati, ...

Usafiri

Mji wa Arusha una kiwanja cha kimataifa cha ndege cha Kilimanjaro inayopatikana kilomita 60 mashariki ukielekea Moshi kwa ajili ya wasafiri wa kimataifa. Kuna ndege za kimataifa na za ndani. Uwanja wa ndege wa Arusha ni uwanja mdogo magharibi mwa mji, kwa sasa wanaendelea na upanuzi wa uwanja huu. Uwanja huu una abiria 87,000 kila mwaka licha ya udogo wake. Mji huu umezungukwa na milima kaskazini na mashariki, na mazingira yake ni mchanganyiko wa misitu ya savanna na misitu mabaki. Hakuna huduma za treni ya abiria kutoka Arusha, lakini kuna makochi (mabasi) ya kwenda Nairobi, Dodoma na Dar Es Salaam pamoja na miji mingine ndani.

Tamaduni

Arusha ni makazi makuu ya sherehe nyingi na sikukuu za Tanzania na tamasha la kila mwaka. Wadhamini wa makampuni mbalimbali husimamia tamasha nyingi kila mwaka. Wasanii kama Shaggy na Ja Rule ni wachache tu ya wasanii maarufu sana duniani waliofanya tamasha katika mji huu.

Kila mwaka maonyesho ya nane nane hufanyika Arusha. Haya huwa maonyesho ya kilimo ambayoo wakulima na wafanyibiashara huja pamoja na kufanya maonyesho, tamasha na burudani. Watu zaidi ya nusu milioni huhudhuria maonyesho haya kila mwaka.

shule

Kuna shule nne za kimataifa ndani na katika maeneo ya Arusha: Shule ya kimataifa ya Moshi (Arusha), Shule ya kimataifa ya Arusha, Braeburn School, na Shule ya Kimataifa ya St Constantine [1] Shule ya St Jude hutoa elimu ya bure kwa watoto kutoka familia za kimaskini sana.

Shule ya kimataifa ya Moshi ilianzishwa mwaka 1969 na sasa ina wanafunzi 460 kutoka mataifa 46. Kuna vyuo vikuu viwili Moshi na Arusha. Chuo cha Arusha kilianzishwa mwaka 1986 na sasa kina wanafunzi 200 wa siku, na hutoa kozi za awali kutoka chekechea hadi darasa la 10. Gredi K-10 kufuata International Baccalaureate mpango wa miaka ya Msingi (PYP) na mpango wa miaka ya Kati (MYP) mitaala kwa maoni ya Afrika na kimataifa. Imekuwa ni moja ya shule za kimataifa za Ib World tangu 2007.

Chuo cha Arcadia hutoa shahada na pia mihula ya muda mrefu na mipango ya majira ya Tanzania, pamoja na mipango ya kuhitimu na kusoma katika Kituo cha Utafiti cha Nyerere kwa ajili ya amani.

Michezo

Timu ya kitaifa cha mchezo wa raga Tanzania hucheza mechi zake za kimataifa mjini Arusha. Michezo ya 2007 Castel Beer Trophy ilifanywa katika mji huu.

Arusha FC, hucheza katika Uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid, huwakilisha mji katika ligi ya mpira wa miguu wa Tanzania.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!