Said anatajwa kuwa mmiliki wa maduka ya Home shopping centre na pia mmiliki wa jengo jipya ambalo limechukua headlines Dar es salaam la Msasani City Mall ambalo ndani yake kuna maduka ya nguo na viatu.. yote yakiwa yanamilikiwa na yeye tu.
Siku kadhaa zilizopita alimwagiwa tindikali na mtu ambae hakufahamika ambapo muda mfupi baadae alikimbizwa hospitali Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ambapo Rais Jakaya Kikwete mtu wa watu ni miongoni mwa waliokwenda kumjulia hali kama unavyomuona kwenye picha.
Moja kati ya Magazeti pendwa wiki hii yalitoa ripoti kwamba Said ndio anatajwa kuwa tajiri kuliko wafanyabiashara wote Kariakoo Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment