Wednesday 3 July 2013

HABARI ZA UMBEYA! STEVEN NYERERE ASEMA WASANII WENZAKE WAMROGA

Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Na Musa Mateja

MAZITO yameibuka baada ya msanii mwenye ‘swaga’ za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, kufungua kinywa na kusema kuwa ugonjwa wake si bure bali amepigwa kipapai.

Akizungumza na paparazi wetu Juni 28, mwaka huu, Steve alisema kuwa kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa ajabu kwa kipindi kirefu sasa na madaktari kushindwa kuelewa kila walipompima, staa huyo anaamini kuwa amerogwa na msanii mwenzake.

“Nimetembea kwa wataalamu wa mambo ya asili na kugundua hilo, sasa ninalazimika kuamini katika imani za kishirikina ingawa ni kitu ambacho muda mrefu nilikuwa nikikipinga sana  lakini kwa hili ninaamini kweli nimechezewa…

SOURCE GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!