MWILI WA DEREVA WA DALADALA
ALIYE FARIKI PAPO HAPO UKIPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI RUFAA
******************************
Watu sita wamefariki Dunia
na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya Barabarani iliyo tokea Nanenane
Darajani eneo la Uyole Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi
Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu
hao kuwa ni pamoja na madereva mmoja wa Hiace.
Masaki amesema dereva wa
Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye kuwa anaendesha Gari nambali
T178 AAV aina ya Toyota Hiace inayofanya kazi Sokomatola na Uyole ambapo muda
huo ilikuwa ikitokea Sokomatola kuelekea uyole.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Maiti nne hazijatambuliwa
hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria katika Daladala hiyo na miili
yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Aidha amesema majeruhi sita
wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo wanawake watano na Mwanamke mmoja .
Ambao mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa
vibaya.
Chanzo cha ajali hiyo
kimetajwa kuwa ni mwendo kasi wa Magari hayo na wito ameutoa kwa Madereva kuwa
makini na kufuata sheria za Barabarani ili kuepusha ajali ambazo zingeweza
kutokea. Ikizingatiwa hilo ni eneo la Jiji.
No comments:
Post a Comment