Tuesday, 4 June 2013

JAJI JOSEPH WARIOBA AZUNGUMZIA MABADILIKO YA KATIBA


 HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE, DAR ES SALAAM

 
 
 

 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.

Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga. Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini

 
Jaji Warioba amesema pia wapo wananchi waliopendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote isipokuwa nafasi ya urais. Jaji Warioba amesema tume ilipitia maoni hayo na kupendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa Mtaa hadi nafasi ya Urais.


Kadhalika Jaji Warioba amesema, Tume pia imependekeza kwamba, mgombea yeyote wa urais ili athibitike kuwa ni mshindi atalazimika kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura, na kwamba endapo mgombea hatafanikiwa kupata asilimia hamsini uchaguzi utarudiwa kwa kuangalia wagombea wawili waliopata kura nyingi.

Mapendekezo mengine yaliyotangazwa na Tume ni pamoja na kuwepo kwa serikali tatu yaani ya Bara,Zanzibar na ile ya Shirikisho.

Pia tume imependekeza kuwa, Bunge la Muungano liwe na jumla ya Wabunge 75, hamsini kutoka Bara, ishirini kutoka visiwani na watano wateuliwe na Rais kutoka makundi maalum ya walemavu.

Mapendekezo mengine ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni pamoja na Rais kubakia na madaraka yake ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu, lakini uteuzi wa ngazi za chini uachiwe Tume ya Utumishi.

Imeeleza kwamba, Rais mara baada ya kufanya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu wakiwemo, mawaziri, manaibu waziri, jaji mkuu na naibu jaji mkuu, viongozi hao watalazimika kuthibitishwa na Bunge 

 

 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!