Sunday 30 June 2013

SERIKALI YASHUSHA USHURU WA PETROLI....USHURU WA SIMU WAFUTWA



MFUMO mpya wa Bunge kuanza na bajeti za kisekta na kumalizia na Bajeti ya Serikali pamoja na uundwaji wa Kamati ya Bajeti, umeonesha makali yake kiasi na kuilazimisha Serikali, kushusha kodi ya petroli na kufuta ushuru wa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu.


Kabla ya Serikali kufikia uamuzi huo jana saa sita usiku, Kamati ya Bunge na wabunge walivutana na Serikali mara kadha wa kadha juu ya kodi mbalimbali, na kulazimika Kamati hiyo na Serikali kukaa si chini ya mara mbili, kujadili.
Katika vikao vyao, vikao viwili vya juzi na jana, Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, naibu wake wawili na wataalamu wake wa wizarani, walikaa kujadili tofauti zao mpaka saa sita usiku.


 
Hoja za wabunge na Kamati ya Bajeti, zilihusu punguzo la kodi katika mishahara, petroli, huduma za simu na magari yenye umri wa kuanzia miaka 10 na kuendelea na kodi katika huduma za utalii.


Hata hivyo, Mgimwa alipokuwa akijibu hoja za wabunge kabla ya kuwaomba wapitishe Bajeti ya Serikali, aliwataka wapitishe kwanza bajeti hiyo na hizo hoja zao zijibiwe katika Muswada wa Sheria ya Fedha, hatua ambayo wabunge waliiridhia na Bajeti ya Sh trilioni 18.2, ikapita.


Hata hivyo baada ya Bajeti kupita, Mgimwa aliwasilisha Muswada huo, ambao uliacha baadhi ya kodi ikiwemo ya magari mabovu kuzidi miaka 10, ya petroli na dizeli na ya simu.


 
Vikao vya saa sita usiku Kutokana na mvutano huo, Waziri wa Fedha na Kamati ya Bajeti walikutana Jumatano wiki hii mpaka saa sita usiku na hata walipotoka, walikuwa hawajaafikiana, kiasi cha Mgimwa kuja na marekebisho kidogo, ikiwemo kuondoa kodi ya utalii, lakini Chenge akaja na msimamo katika kodi ya petroli na utumaji na upokeaji fedha kwa njia ya simu.


 
*Suluhu
Kabla ya Mgimwa kutangaza mwafaka, Chenge alipewa nafasi na kumsifu Waziri Mgimwa kwa kuwa msikivu na mtu asiyependa makuu na kusema, wamefikia makubaliano ambayo ni habari njema kwa Watanzania.

Baada ya Chenge kutangaza habari hiyo njema, Mgimwa alisimama na kuanza na kodi ya petroli, ambapo alisema Serikali imeridhia kutoongeza ushuru wa bidhaa katika petroli wa Sh 61 na hivyo, itaendelea na ushuru uliopo wa Sh 333.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!