Kamati ya msiba ya mwanamuziki Albert Mangwea, imeleta taarifa kwamba mwili wa Ndugu yetu Albert Mangwea hautoweza kufika siku ya jumapili ya tarehe 2/ 06/2013 kama ilivyo taarifa hapo awali, hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.
Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi wetu waliopo nchini Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza tushirikiane na uvumilivu kwa hili.
No comments:
Post a Comment