Pages

Saturday 11 May 2013

WASIOTOA MSAMAHA WA MATIBABU YA AFYA, KUSHUGHULIKIWA IPASAVYO..

Hussein-Mwinyi NA MAGREGH KINABO – MAELEZO DODOMA 
SERIKALI imewaagiza watendaji na wananchi kupitia kamati za o za afya kuhakikisha misamaha inatolewa kwa wote wanaostahili.
Aidha imesema kuwa  kituo ambacho hakifanyi vizuri katika ukusanyaji na udhibiti  wa matumizi ya fedha  zinazotokana kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), viongozi husika wapewe onyo. Baada ya muda watakaopewa iwapo hakuna mabadiliko  zichukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa madaraka waliyopewa.
Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi  wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi  wakati akifungua mkutano  wa mkutano mkuu wa mwaka  wa  waganga wakuu wa mikoa , wilaya na baadhi wa wakurungezi wa hospitali za rufaa na taasisi za wizara hiyo wakiwemo wakurugnezi wa asasi za kiraia, wadau wa maendeleo na washiriki kutoka  Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).
Mkutano huo wa siku tatu umefanyik katika  ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment