Pages

Friday 3 May 2013

MAJAMBAZI YAUAWA WAKATI YAKIPAMBANA NA POLISI HUKO MBEYA. ...........tunaomba radhi kwa picha hizi........





Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha
Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu

 Wakati polisi nchin i wakiendelea kutafuta  suluhisho la kupambana na vitendo vya ujambazi nchini,  Mkoa wa  Mbeya umezidi umeshika usukani kwa ongezeko kubwa la ujambazi mkoani humo ambapo hivi punde   watu watano wanaodhahaniwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoni humo


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio.....


Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.

Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba
wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio.....


Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.

Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya
Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana mara moja ambapo miili  yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
habari na picha kwa hisani ya Mbeya yetu.

No comments:

Post a Comment