Friday 26 April 2013

WABUNGE KUTORIDHIKA NA BAJETI YA WIZARA YA MAJI



Bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka wa fedha 2013/14, iliyokuwa ipitishwe na Bunge jana, imekwama na kuahirishwa hadi Jumatatu.

Hatua hiyo ilifikiwa, baada ya wabunge kutoridhika na kiwango cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya wizara hiyo.
 

 Wakati wabunge hao wakichangia hoja zao katika mjadala wa bajeti hiyo, iliyowasilishwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe juzi, walionesha msisitizo kuwa hali ya upatikanaji wa maji ni mbaya nchini.
 
 
 Spika wa Bunge, Anne Makinda ndiye aliyeahirisha kupitishwa kwa bajeti hiyo, wakati akitoa majibu ya Mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba (CCM).

Ni kweli suala la maji hatuwezi kulifanyia utani, sasa naitaka Wizara ya Maji, Kamati ya Bajeti na Wizara ya Fedha, zikafanyie kazi suala hili, walete majibu ya uhakika hapa Jumatatu,” alisema Makinda.
 

 Alisema amefuatilia na kubaini kuwa idadi kubwa ya wabunge waliochangia mjadala huo wa maji, wamekataa kuiunga mkono Bajeti hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa kushughulikia suala hilo kwa utaratibu wa majadiliano ambao Bunge hilo limeridhia

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!