Wednesday 3 April 2013

MWANAMICHEZO WA WIKI-DIDIER DROGBA


Didier Yves Drogba Tébily ni mchezaji wa timu ya Galatasaray ya Uturuki. Drogba ni kapteni wa timu ya taifa ya Ivory Coast.

Akiwa na timu ya Chelsea,Drogba ndiye mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote kutoka  nje.

Didier Drogba alizaliwa Abidjan, Ivory Coast.

Drogba amemwoa Diakite Lalla,mwanamke kutoka Mali ambaye walikutana Paris. Drogba na Diakite wamejaliwa kupata watoto watatu. Drogba ana wadogo zake wawili wa kiume, Joel na Freddy Drogba ambao nao ni wachezaji wa mpira wa miguu.

Drogba amekuwa mtu muhimu katika kuleta amani nchini mwake.

Mwaka 2011, Drogba alijiunga na Tume ya upatanishi na usuluhishi kama mjumbe na kusaidia upatikanaji wa amani nchini kwake.(Ivory Coast)
CHINI:Picha mbalimbali za Drogba

Drogba akiwa na mkewe


Mke wa Drogba na watoto wao

Drogba ndani ya jezi ya Galatasaray

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!