Monday 29 April 2013

KENYA YAIPONGEZA NA KUISIFU KAMPUNI YA MC DONARD LIVE LINE TECHNOLOGY YA TANZANIA

 
Mmiliki wa Kampuni ya McDonald Live Line Technology, McDonald Mwakamele (kulia) akiwaonesha maofisa kutoka Kampuni ya Umeme ya Kenya (KPCL), vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza umeme bila kuuzima walipotembelea chuo cha kampuni hiyo, mwanzoni mwa wiki, wilayani Mvomero, Morogoro. Kenya iko mbioni kuingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya mafundi wao kufundishwa teknolojia hiyo ya kisasa. Kutoka kushoto ni maofisa wa KPCL, Meneja Uendeshaji, Noah Ogano, Peter Waweru na Mhandisi Charles Mwaura ambaye ni Naibu Meneja Huduma za Kawaida.
Mcdonald Mwakamele akiwaonesha maofisa wa KPCL, baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kazi hiyo
 
Mwakamele akiwa juu ya nguzo akionesha jinsi ya kutengeneza umeme bila kuukata
 
Shirika la Umeme nchini Kenya(KPLC), limeeleza kuwa linaangalia namna ya kuingia makubaliano ya wataalamu wake kuja nchini Tanzania ili kujifunza kutumia teknolojia ya kufanya matengenezo ya umeme bila kuukata
 
Hayo yamesemwa wiki hii mkoani Morogoro walipotembelea kampuni pekee Afrika Mashariki na Kati inayoweza kutengeneza umeme bila kuukata ya McDonald Liveline Technology, walisema wamefurahishwa na teknolojia hiyo na imebaki kwao kuamua ni wataalamu wangapi wajifunze kwa maslahi ya nchi yao.

 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!