Unaweza kutengeneza supu ya karoti kwa kuchemsha vipande vyake na nyanya. Chukua karoti na nyanya ulizochemsha, kisha weka kwenye ‘blender’ au chombo kingine unachoweza kusagia. Saga mchanganyiko huo ili kupata supu, unaweza kuongeza viungo vingine ili kupata ladha. Unaweza pia kuinywa ikiwa ya moto au ikiwa imepoa, pia karot inaweza kuliwa kama ilivyo
Kuna kitu kinaitwa beta-carotene ambayo imo ndani ya karoti na hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamini A. Vile vile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa kukinga kuta za utumbo.
Karoti ikitumiwa vizuri na tena mara kwa mara inasaidia kukinga na kuponya magonjwa yafuatayo: macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu, ngozi, kupunguza tindikali inayodhuru tumboni na kukinga magonjwa yenye asili ya kansa.
No comments:
Post a Comment