Nyumba kandokando ya mto Pangani
Kivuko kikivusha wakazi kutoka Pangani mjini kwenda kijiji
cha Bweni
Ni muhimu
kutembelea miji ya kihistoria katika nchi yetu. Je,unajua umuhimu wa mji wa
Pangani?
Mto Pangani umeigawa Pangani katika sehemu mbili,Pangani
mjini na kijiji cha Bweni
Pangani ilikuwa
ni ngome kuu ya upinzani dhidi ya utawala wa Wajerumani ambapo Abushiri bin
Salim al-Harthi aliongoza upinzani huo.
Pangani ilikuwa
kitovu cha biashara ya watumwa.
Pangani ni wazalishaji wakubwa wa nazi na popoo(betel
nut) na vilevile ni mji wa uvuvi.
Pangani ni
kivutio kikubwa kwa utalii kwa kuwa na pwani nzuri na hifadhi ya taifa ya
SADANI ambayo ipo katika pwani.
TUTEMBEE ILI KUONA VIVUTIO VILIVYOPO NCHINI MWETU.
No comments:
Post a Comment