Lionel Andres Messi ni mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya Barcelona mwenye asili ya Argentina.
Lionel alizaliwa Rosario, Santa Fe Province. Wazazi wake ni Jorge Horácio Messi, mfanyakazi katika kiwanda cha chuma na Celia Maria Cuccittini. Baba yake Messi ana asili ya Italia katka mji wa Ancona.
Messi ana kaka wakubwa wawili, , Rodrigo na MatÃas, na dada, MarÃa Sol.
Akiwa na umri mdogo,Messi alihamia Hispania kutokana na matatizo ya kiafya.
Mwaka 2007, Messi alianzisha mfuko kwa jina Leo Messi Foundation.Mfuko huu ni kwaajili ya kusaidia upatikanaji wa elimu na huduma za afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Kutokana na matatizo ya matibabu aliyoyapata Messi utotoni, Leo Messi Foundation imetoa ufadhili wa matibabu kwa watoto wa Argentina waliokutwa na magonjwa kwa kuwapeleka Hispania. Leo Messi Foundation inagharamia fedha za usafiri, matibabui na malazi.
Mwaka 2010 Messi alichaguliwa kuwa goodwill ambassador wa UNICEF. Messi amelenga kupigania haki za watoto.
Machi 2013, Messi amechangia euro 600,000 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya watoto katika mji atokao, Rosario, Argentina.
Desemba 2012, timu ya FC Barcelona ilitangaza kuwa Messi atasaini mkataba wa miaka 5 (mitano) ambao utamweka Barcelona hadi mwaka 2018 na mshahara wake kupanda kuwa euro millioni 16 sawa na dola millioni 21.2 hivyo kumfanya awe ndiye wa soka mchezaji anaelipwa pesa nyingi zaidi.
Hayo ndiyo machache kuhusu mchezaji wetu wa wiki ,Lionel Andres Messi
No comments:
Post a Comment