Monday, 10 April 2023

MWIMBAJI GWIJI WA MUZIKI WA DANSI HUSSEIN JUMBE AMEFARIKI DUNIA

Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound,  amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo. 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!