Ni Vizuri kiafya kutumia tunda kama lilivyo na sio juisi yake.
Ingawaje hili limepotoshwa na waelimishaji baadhi wanaijengea jamii fikra mbaya na angamizi kwamba "Juisi za matunda asili ni mbadala wa Soda na Juisi za Kusindika" Uongo Mkubwa sana hata kama Ukitumia Juisi asili za Matunda bado Utakua hujajikinga na magonjwa ya lishe.
"Lengo la Kuituhumu soda na Juisi za kusindika kuwa ni vibaya kwa afya ni kwa sababu vinatuhatarisha na maradhi ya lishe"
.
Wapi palipo andikwa kwamba mtu mwenye uzito sahihi akinywa Juisi za matunda badala ya juisi za kiwandani zitamkinga na maradhi ya lishe?
.
Ndio huo usemi kwamba "Kula matunda kwa Wingi Kunasaidia Kuimarisha afya yako"
.
Una Kitambi, Una Kisukari, Una mvurugiko wa Homoni, Una shinikizo la damu, Una Vidonda vya tumbo, Una Kiungulia na Kubeuwa. Je ukinywa Juisi za matunda kwa wingi utapona? Hakika Utaongeza Maradhi yako.
.
Achana na usemi "Kula matunda kwa wingi ni afya" Chukua usemi huu "Kula matunda kwa akili".
.
Aina na wingi wa matunda inategemea na hali yako kiafya uliyo nayo na Malengo yako unayotaka kuyafikia.
.
Mimi daktari nitakuwa wa ajabu Nimshauri mtu mwenye kitambi au Kisukari atumie matunda mengi kuimarisha afya yake au Nimshauri anywe juisi za Matunda asilia bila kuweka sukari Eti atapona maradhi yake. Nitakua Namuonjesha Kifo nakwambia.
.
Kuwa na Kitambi ni Hatua za awali za maradhi sugu ya lishe. Ni mpasuko wa Msingi wa afya yako. Ina ashiria kuna Kitu kinajitengeneza. Hata kama sasa Unajipima huna maradhi yawezakuwa vipimo unavyopima ni Vidogo uwezo wa kugundua maradhi katika hatua za awali ni Mdogo sana.
.
Kiafya Mwili Umetengenezwa kujiendesha katika kiwango kidogo sana cha sukari. Sukari Kawaida inatakiwa Isome 100mg/dl sawa na 5.6mmol/L haitakiwi kuzidi 6 ukiwa hujala chochote. Kiwango hicho cha 5.6mmol/L ni sawa na Kijiko 1 cha sukari (gram 5) za sukari kwenye Lita 5 za damu ya mtu mzima. Kawaida sukari inatakiwa kusoma Kijiko 1 mpaka 2 kwenye lita 5-7 za damu.
Sukari yoyote ya ziada unayo Umiminia Mwili Inatakiwa isafishwe haraka sana kwenye damu kwenda katika mfumo wa hazina. Sukari hio ya ziada huhifadhiwa katika matenki mawili ya kuhifadhi sukari ya ziada ambalo ni GLYCOGEN na MAFUTA.
Ina maana kadri unavyo Jimiminia Mi Juisi ya Matunda mwili hawa unamchakato Uleule wa Kushughuliki sukari bila kujali chanzo (Iwe asili au Kutoka kwenye Vyanzo vya Kusindika) mchakato ni Sukari yoyote ya ziada itasukumwa kwenda kwenye Hazina Inaitwa Mafuta na Glycogen.
.
Homoni inayo Shughulikia Ile sukari ya ziada Insulin huitwa Anabolic homoni maana yake Inaruhusu Kitendo cha Kuhifadhi tu na Hairuhusu Kutumia. Ina maana Kwamba Ile sukari Iliyo hifadhiwa katika mfumo wa mafuta na glycogen haiwezi kutumika mpaka kuwepo na Uhaba wa sukari.
.
Ili kuunguza mafuta ambayo ni hazina ya sukari ya ziada ambayo huwa haina ukomo. Unatakiwa uweke mwili wako kwenye mazingira ya kutokula kwa muda wa masaa zaidi ya 8 mpaka 12. Kwa maana hio Watanzania wengi huwa tunakula chakula kinacho fuata kabla haya mwili haujaanza kutumia hazina ya sukari uliyohifadhi baada ya mlo uliopita. Kwa sababu wengi tunakula milo 3 kwa siku na wengine milo mingi zaidi wanashinda wanatafuna vitu au wanakunywa vimiminika vyenye Sukari.
Kwa maana hio Ukitumia Tunda lenyewe utaingiza sukari kidogo kuliko ukikamua tunda lenyewe mpaka upate juisi nzuri utakayokunywa glasi nzima nafsi yako isuuzike.
Matumizi mabaya ya sukari Mojawapo ni Kukamua Juisi za matunda asili badala ya Kula matunda kama Yalivyo.
.
SOMO LIJALO NITAFUNDISHA KWAMBA UNYWAJI WA JUISI ZA MATUNDA ASILI HAUKUONGEZEI FAIDA YA VITAMINS KULIKO YULE ATAKAYE KULA TUNDA LILIVYO.
Andika Maoni Yako Hapa HII NDIO SABABU WATU WANAPATA NON ALCOHOLIC FATTY LIVER WAKATI HAWANYWI POMBE NA HAWANYWI SODA SABABU KUU UNAZIDISHA VIMIMINIKA VYA SUKARI VITOKANAVYO NA KUKAMUA MATUNDA ASILIA.
No comments:
Post a Comment