Tuesday 4 May 2021

Tajiri mkubwa duniani Bill Gates na mkewe wameachana Baada ya kuishi kwa muda wa miaka 27 katika ndoa

"Baada ya majadiliano ya muda mrefu na kufanya jitihada kubwa juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kuvunja ndoa yetu." Hayo ni maneno kwenye ujumbe wa barua iliosambazwa kuashiria mwisho wa ndoa ya Bill Gates na mkewe Melinda French.


Baada ya kuishi kwa muda wa miaka 27 katika ndoa na kujenga kampuni zenye mafanikio makubwa sana ndoa yao imefika ukingoni. Katika ujumbe uliopostiwa kwenye mtandao wa Twitter wawili hao wameeleza kuwa "hatuamini tena kama sisi tunaweza kukua pamoja kama wenzi katika awamu hii inayofuata ya maisha yetu"
Bill Gates alimuoa Melinda French mwaka 1994. Wameishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 27. Katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto watatu. Inadaiwa wawili hao kabla ya kufunga ndoa walikuwa na makubaliano ya namna ya kugawana mali zao ikitokea wameachana. Ndoa ya hawa matajiri wakutupwa wa dunia imekufa...kwa sasa Bill Gates ana umri wa miaka 65 na Melinda ana miaka 56.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!