Monday 15 February 2021

Liberia Yatangaza Tahadhari Mlipuko wa Ebola

 



RAIS wa Liberia, George Weah,  ametangaza kuziweka mamlaka za afya za nchi hiyo katika kiwango cha juu cha tahadhari baada ya watu wanne kufariki dunia kwa ugonjwa wa Ebola kwenye taifa jirani la Guinea.

 

Weah ameamuru mamlaka za afya za Liberia kuongeza ufuatiliaji wa karibu wa hali inayoendelea pamoja na kuchukua hatua za udhibiti kufuatia ripoti ya kuzuka homa ya Ebola nchini Guinea.

 

Kwa mujibu wake, vifo vya watu hao wanne vimetokea kwenye mji wa Gouecke uliopo nchini Guinea karibu na mpaka wa kaskazini-mashariki mwa Liberia.

 

Mapema leo waziri wa Afya wa Guinea, Remy Lamah, alithibitisha kuwa watu wanne wamekufa kwa Ebola, ikiwa ni vifo vya kwanza vya maradhi hayo tangu kutokea mlipuko mkubwa wa mwaka 2013 hadi 2016.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!