Tuesday 26 January 2021

Ngoja nikupe story fupi....

 


Ngoja nikupe story fupi....


"Kijana mmoja alienda kwa mtabiri wa mambo ya mbeleni ili apate kufahamu 'future' yake ikoje.

Baada ya kufika na kuzungumza na yule mtabiri, kijana alicholewa Maduara mawili. Moja lilipakwa rangi nyeupe na jingine nyeusi.

Kisha, yule mtabiri akaweka mdudu jongoo katikati ya yale maduara mawili. Halafu, akamwambia yule kijana, "Endapo jongoo huyu atatambaa kuelekea liliko duara jeupe, kesho yako itakuwa yenye heri, utafanikiwa kwa kila jambo utakalokua ukifanya.

Lakini, endapo jongoo huyu atatambaa kuelekea liliko duara jeusi, basi umekwisha. Hauna 'future' yoyote na maisha yako yatakuwa ya tabu.

Baada ya yule mdudu kuwekwa katikati ya zile duara mbili, alianza kutambaa kuelekea liliko duara jeupe.

Kijana akafurahi mno moyoni.

Baada ya kukaribia tu kuingia duara jeupe, yule mdudu akasimama ghafla. Kisha, akageuza na kuanza kuelekea liliko duara jeusi.

Yule kijana huku akiwa ameshikwa na hofu akatazama yule jongoo akilielekea duara jeusi. Kule ambako anaambiwa hakuna 'future' na maisha ni ya tabu.

Kisha, wakati jongoo akiwa amekaribia kuingia duara jeusi, yule kijana akanyosha mkono wake, akamshika yule jongoo, akamuinua na haraka haraka akamuangushia katika duara jeupe.

Yule mtabiri akashangaa, maana, hajawahi kuona hata siku moja mteja wake akifanya jambo kama lile la kuingilia kazi yake.

Akamuuliza yule kijana kwanini amefanya vile?

Yule kijana akatabasamu. Kisha akamwambia, "Siwezi kukaa hapa na kushuhudia ndoto zangu zikiharibika wakati naweza kufanya jambo kuokoa ndoto hizo. Ndoto zangu na kesho yangu ipo mikononi mwangu. Mikono yangu itaamua nifeli ama nifanikiwe.

Akainuka na kuondoka zake.

Nini dhima ya kisa hiki?

Mwaka huu 2019, Inuka. Usikae chini na kutazama ndoto zako zikielekea kufa. Zinyanyue ndoto zako na zipeleke katika duara la mafanikio. Kule ambako wewe unahitaji kufika.

Nguvu na uthubutu wa kufanya hivyo upo mikononi mwako. Sasa, chagua mawili, ukae chini uendelee kulalamika, kuumia, kuhuzunika huku ukidhani kuna mtu ndio amebeba ndoto zako ama uinuke na kupigania furaha yako.

Huu sio mwaka wa kukaa na kutegemea miujiza. Bali ni mwaka wa kutengeneza miujiza. Tengeneza Miujiza yako. Amini katika uwezo wako. Na kwa msaada wa MUNGU utafanikiwa

IMEANDIKWA NA TITO CARLOS:

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!