Hii ni habari njema:
Marekani imeidhinisha dawa ya VVU itakayo kuwa inatumiwa kwa mwezi mara 1.
Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa ya Marekani imeidhinisha dawa mpya ya kupambana na virusi vya UKIMWI itakayokuwa ina tumika mara moja kwa mwezi. Dawa hiyo iitwayo Cabenuva itakuwa inatolewa kwa njia ya Sindano.
Wagonjwa wanaostahili kutumia dawa hiyo ni wale ambao wamedhibiti kiwango cha virusi kwenye damu zao kutokana na dawa wanazotumia kwa sasa, wale ambao matibabu wanayotumia hayajashindwa kufanya kazi pamoja na hawana usugu dhidi ya dawa hiyi pamoja na aleji. Pia FDA imeidhinisha dawa aina ya kumeza aina Vocabria ambayo itakuwa inatumika mwezi mmoja kabla mgonjwa hajaanza kutumia dawa ya Sindano ili kujua kama inamletea madhara yoyote.
Kwa sasa watu wanaoishi na VVU wanalazimika kumeza dawa kila siku. Dawa hii italeta unafuu kwa wagonjwa wataohitaji kutumia dawa mara moja kwa mwezi na wametimiza vigezo. Hata hivyo dawa hiyo ni kwa ajili ya watu wenye maambukizi ya aina moja tu ya VVU (HIV type 1).
No comments:
Post a Comment