Friday 18 January 2019

Ugonjwa Wa Tetanus Ni Nini?


umeshashuhudia watu wengi wamekufa na tukaambiwa wamekufa kwa tetanus. Maneno kama tetanus haina tiba au ukiumwa tetanus unaganda shingo ni ya kawaida. Kwamba ukijichoma na kitu chenye ncha kali chenye kutu, uwahi ukachomwe sindano ya tetanus. Lakini, tetanus ni ugonjwa gani hasa?

Mada yetu ya leo itauchambua ugonjwa huu wa tetanus ili uweze kujua chanzo cha tetanus, dalili zake, tiba au kinga ya tetanus. Bila kupoteza muda, tuanze mara moja.
Tetanus Ni Nini?
Tetanus ni ugonjwa mkali, ambao mara nyingi unaua wa mfumo wa neva unaosababishwa na sumu zinazotengenezwa na bakteria aitwaye Clostridium tetani. Bakteria huyu hupatikana kwenye udongo na kwenye utumbo wa binadamu na wanyama (kinyesi). Baketria huyu huweza kuwa kimya kwa miaka mingi kama spore kabla ya kuzinduka na kugeuka bakteria anayezaliana.
Bakteria huyu huzaliana kwenye kidonda. Vidonda vyenye kina au vile vyenye tishu zilizokufa ndiyo maeneo ambayo bakteria huyu anaweza kuingilia kirahisi mwilini.
chanzo cha tetanus
Vidonda vinavyotokana na kujitoboa kama vile vya misumari, vibanzi au vipande vya vioo vyenye ncha kali, vidonda vya upasuaji, vidonda vya kupigwa risasi au vya kuumwa na wadudu ndizo sehemu ambazo bakteria huyu hupata nafasi ya kuingia katika mwili. Bakteria huyu anaweza pia kupitia vidonda vya kuungua na moto na matundu ya sindano. Tetanus inaweza kuwa hatari kwa mama na mtoto mchanga (kupitia uterus baada ya uzazi na kupitia kwenye kitovu).
Sumu kali (tetanospasmin) inayozalishwa wakati bakteria hawa wanazaliana ndicho chanzo cha madhara makubwa ya tetanus.
Sumu za tetanus huharibu mawasiliano baina ya neva na misuli unaoamshwa na neva hiyo, na hasa sehemu vinapokutana (neuromuscular junction). Sumu za tetanus hukuza ishara za kikemikali kutoka kwenye neva kwenda kwenye misuli, hali inayosababisha misuli kukaza moja kwa moja.
Dalili Za Tetanus
Tetanus huchukua muda wa wastani wa kati ya siku 2 hadi miezi miezi 2 kuanza kuonyesha dalili zake, lakini kwa kawaida ni katika siku 14 toka siku ya kupata jeraha. Dalili za kawaida ni:
. Kukaza kwa misuli kwenye taya (trimus)
. Ugumu wa misuli ya shingo
. Shida wakati wa kumeza
. Ugumu wa misuli ya tumbo
. Mikazo ya misuli inayodumu kwa dakika kadhaa, mikazo ambazo inasababishwa na vitu vidogovidogo kama sauti kubwa, kuguswa au mwanga.
Dalili nyingine zinaweza kuwa:
. Homa
. Jasho kali
. Kupanda kwa pressure
. Mapigo ya moyo kwenda mbio
Katika siku saba za mwanzo baada ya maambukizi ya bakteria, kukaza kwa misuli kunakosababishwa na sumu za tetanus kwenye eneo la kidonda kutasambaa hadi sehemu nyingine zote za mwili. Kukosa utulivu na maumivu ya kichwa vitaonekana. Hii itahusisha misuli yote ya mwili ikiwa ni pamoja na misuli muhimu inayohusika na upumuaji. Misuli hii ya upumuaji inapokosa nguvu, kupumua inakuwa ni shida au haiwezekani na kifo kinatokea endapo msaada wa kuokoa maisha utakosekana. Pamoja na vifaa vya kusaidia upumuaji, maambukizi kwenye njia za hewa ndani ya mapafu yanaweza kusababisha kifo.
Kinga Ya Tetanus
Njia bora kabisa ya kupambana na tetanus ni kuizuia. Sumu za tetanus zikishanata kwenye maeneo zinapoishia neva, hakuna njia za kuziondoa. Ili kupona kutokana na sumu ya tetanus inabidi neva mpya ziote, tendo ambalo linalochukua hadi miezi kadhaa.
Unaweza kujikinga na tetanus kirahisi sana kwa kutumia chanjo.
Watoto wote wanatakiwa wapewe chanjo ya tetanus, kuanzia wanapokuwa na miezi 2 na kuimaliza wanapofikia miaka 5. Sindano za ziada (Booster vaccination) zinapendekezwa wanapofikia miaka 11.
Baadaye wanatakiwa kupata chanjo (follow-up booster vaccination) kila baada ya miaka 10.

Tiba Ya Tetanus

Ugonjwa wa tetanus hauna dawa.
Tiba hutolewa ili kuwaua bakteria kwa kutumia antibiotics wakati mgonjwa akichunguzwa juu ya dalili zo zote za kushindwa kupumua. Tiba inalenga kuzuia utengenezwaji wa sumu, kupunguza makali yake, na kudhibiti mikazo ya misuli.
Hali ikiwa mbaya zaidi, mgonjwa atapewa vifaa vya kumsaidia kupumua.

Sumu inayozunguka ndani ya mwili itaondolewa kwa kutumia antitoxin drugs. Sumu ya tetanus haisababishi madhara ya kudumu kwenye mfumo wa neva. Baada ya kupona, mgonjwa bado atatakiwa kupata chanjo dhidi ya tetanus.

1 comment:

Leona Knight said...

I was diagnosed of Herpes 2 years ago and I have tried all possible means to get the cure but all to no avail, until I saw a post in a health forum about a Herbal Doctor(Dr Akhigbe) who prepares herbal medicine to cure all kind of diseases including Herpes, at first i doubted, if it was real but decided to give him a trial, when I contacted Dr Akhigbe through his Email: drrealakhigbe@gmail.com he guided me and prepared a herbal medicine and sent it to me via courier Delivery service,when I received the package (herbal medicine) He gave me instructions on how to consume it,I started using it as instructed and I stopped getting outbreaks and the sores started vanishing, could you believe I was cured of this deadly virus within two to three weeks and notices changes in my body. Days of using this REMEDY,couldn't believe the healing at first until I see it as my HERPES  get cleared like magic Dr Akhigbe also use his herbal medicine to cure diseases like, HIV, HERPES, CANCER, ALS, CHRONIC DISEASE, HEART DISEASE, LUPUS, ASTHMA,  DIABETES, MAR-BURG VIRUS,  HEPATITIS A AND B.ECZEMA, BACK PAIN, EXTERNAL INFECTION ,ASTHMA, MALARIA, DENGUE FEVER, BACTERIA DIARRHEA, RABIES, OBESITY, PROGENITOR,  MENINGITIS, ARTHRITIS, EPILEPSY,STROKE, LYMPH EDEMA, GALLSTONE, DICK AND BREAST ENLARGEMENT, PULMONARY HYPERTENSION, PENIS  EJACULATION, ,   HPV, DICK ENLARGEMENT, IMPOTENCE, DENGUE, TETANUS, CORNELIA DISEASE, OSTEOPOROSIS, RHEUMATISM, THYROID, COLD & FLU,KIDNEY DISEASE,ACME. PROTOPLASMIC  ERYSIPELAS. etc Contact this great herbal Doctor today the father of herbal root cure. via Email: drrealakhigbe@gmail.com or whatsapp him  +2349010754824   and get cured permanently He is real..website:      https:drrealakhigbe.weebly.com

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!