Thursday 20 September 2018

Kivuko cha MV Nyerere chazama, yadaiwa watu kadhaa wamepoteza maisha

capture-png.872210
 Watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKALA wilayani Ukerewe.


====

Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere 


dnip_wvx0aadkus-jpg.872340

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.

Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.

Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.



babd97c8-0a0a-45d2-acca-89d2224fa5ce-jpg.872299

dnitylxwwaedlus-jpg.872676
 
Wanajeshi na raia wakitoa msaada wa uokoaji​


KWA HISANI YA JMF

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!