Tuesday 31 July 2018

MWACHE AENDE!

Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia kufika mwisho pale umpendae anapoamua kukuacha. MUACHE AENDE!


• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe mtu akupende, mwache mwenyewe akupende kutoka moyoni mwake, kama hakupendi... MWACHE AENDE!
• Wewe ni wa thamani mno, si mtu wa kulilia penzi kiasi hicho. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku_treat kama uchafu. Kama atakuchukulia kuwa unajipendekeza.. MUACHE AENDE!
• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi kwa mtu ambae hakutaki. Kuna mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kuomba kum_bembeleza mtu asiekutaka! Kwanini? MUACHE AENDE!
• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi MUACHE AENDE!
• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo. MUACHE AENDE!
• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu.
MUACHE AENDE!
Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe.
Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano. Ni ngumu sana ila kwa mustakabali wa furaha yako ya sasa na ya baadae, mimi nakwambia MUACHE AENDE.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!