Monday, 11 June 2018

Wanaume kuongezewa muda wa likizo ya uzazi nchini

Leo June 11, 2018 kuna hii ya kuifahamu kutoka Bungeni ambapo Serikali imesema inaandaa utaratibu utakuowezesha kuongeza muda wa likizo ya uzazi kwa akina mama walioajiriwa ambao watajifungua watoto kabla ya wakati, ili kusaidia kutenga muda wa kutosha kwa wazazi kuwa karibu zaidi na watoto hao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu, Jenista Mhagama, amesema kuwa Serikali imepokea maombi mengi kuhusu jambo hilo na kuongeza kwamba likizo hiyo haitawanufaisha akina mama pekee bali hata wazazi wakiume wa watoto hao.
“Naomba nilihakikishie Bunge lako tukufu kuwa, hayo ni mambo ambayo yanaendelea kujadiliwa na kufanyiwa kazi ili kuweza kuwasaidia wanawake lakini hata wanaume ambao wake zao wamejifugua watoto ambao wamezaliwa kabla ya umri wao, ili waweze kupewa haki na kusaidia malezi ya watoto na malezi ya familia kwa ujumla” Waziri Mhagama

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!