Tuesday 15 May 2018

WATUHUMIWA 6 KATIKA KESI YA MAUAJI YA MFANYABIASHARA ERASTO MSUYA WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU


Watuhumiwa 6 katika kesi ya mauaji ya Mfanyabiashara Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya wamekutwa na kesi ya kujibu huku mtuhumiwa mmoja, Jalila Zuber (28) akionekana hana kesi ya kujibu na kuachiliwa.


Uamuzi huo umetolewa siku ya leo Mei 14, 2018 na Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi.

Waliokutwa na kesi ya kujibu ni Sharifu Mohamed (31), ambaye ni mfanyabiashara wa madini na mchimbaji mdogo, mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Shaibu Jumanne maarufu kama “Mredii” (38), mkazi wa Songambele, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara na Mussa Mangu (30), anayeishi Shangarai kwa Mrefu.


Wengine ni Sadick Jabir maarufu “Msudani” (32), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata, Wilaya ya Hai, Karim Kihundwa (33), mkazi wa Lawate, Wilaya ya Siha na Alli Musa maarufu “Mjeshi”, mkazi wa Babati, mkoani Manyara.

Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi 22, Agosti 7, mwaka 2013, saa 6:30 mchana katika eneo la Mijohoroni, kando kando ya barabara kuu ya Arusha-Moshi, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!