Wednesday, 23 May 2018

MTWARA: Watoto wawili wa miaka 8 na 12, waopoa mwili wa Mzee aliyekufa maji

Image may contain: 1 person, sitting and outdoor

Watoto wawili umri wa miaka 8 na 12, wameibuka mashujaa baada ya kuopoa mwili mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mzee Nampwenge aliyekufa maji, baada ya kuzama kwenye bwawa alipokuwa akiogelea huko Namanyanga, Naliendele mkoani Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa mtaa wa Namanyanga Ally Salum Nayove amesema ni kweli watoto hao waliotambulika kwa majina ya Faraji Muhibu darasa la nne na Islam Shaibu darasa la pili ndio waliojitosa kwenye bwawa lililojaa maji kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha na kuutoa mwili huo.

Naye Mzee Hamisi Nahoda ambaye ni rafiki yake wa karibu wa Mzee Nampwenge aliyekuwa naye siku ya tukio wakiogelea, amesema kwamba rafiki yake alikuwa akijikumbusha kuogelea lakini maji yalimzidi na kufariki dunia saa chache kabla ya kufuturu.

Kutokana na tukio hilo Mwenyekiti Ally Salum Nayove amewataka wananchi na watoto wadogo kutocheza katika maeneo hayo, ambayo awali yalikuwa ni machimbo ya mchanga na sasa kujaa maji kutokana na mvua. 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!