Saturday 24 February 2018

Uhamiaji: Vibali vya wafanyakazi waliokamatwa Kiu vinahakikiwa

IDARA ya Uhamiaji nchini imesema itawachukulia hatua raia wa kigeni waliokamatwa katika Chuo Kikuu cha Kampala (Kiu) bila kuwa na vibali vya kuwepo nchini baada ya kukamilika kwa uhakiki wa hati zao.


Raia hao 48 walikamatwa Februari 20 baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kufanya ziara chuoni hapo akiambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala na kubaini madudu ikiwemo uwepo wa wafanyakazi wanaofanya kazi bila kuwa na vibali. Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Idara hiyo, Ally Mtanda alisema bado wanaendelea kuwashikilia raia hao ili kuhakiki taarifa zao na kubaini ni wangapi wanafanya kazi kwa vibali halali.
Alisema raia 21 kati ya 48 waliodai wana vibali halali vya kufanya kazi wanaendelea kuhakikiwa na watakapokamilisha watakaobainika kuishi nchini kinyume cha sheria watachukuliwa hatua. Alisema raia hao 48 waganda ni 30, Nigeria watano, wa Kenya wanne na kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa mmoja na Watanzania sita ambao walikataa kutoa ushirikiano kwa maofi sa wa uhamiaji. Mtanda alisema wanategemea kukamilisha uhakiki wiki hii na watakapokamilisha kuchambua taarifa za wahusika watakaobainika kuishi kinyume cha sheria watawachukulia hatua ikiwemo kuwafi kisha mahakamani na kuwaondoa nchini kama sheria inavyosema.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!