Thursday 16 November 2017

Mugabe agoma kung'oka

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ameendelea kusisitiza kwamba yeye bado ni kiongozi 
halali wa nchi hiyo na kukataa upatanishi unaofanywa Kasisi mmoja wa Kanisa 
Katoliki ili kuwezesha mabadiliko ya uongozi kwa njia amani baada ya jeshi kuchukua

udhibiti tangu siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa vyanzo vya intelijensia nchini humo, Kasisi Fidelis Mukonori, amejitolea kuwa mpatanishi kati ya Majenerali wa Jeshi na Rais Mugabe, ingawa hakuna taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo yenye lengo la kuepusha umwagaji damu baada ya Mugabe kuondoka madarakani.
Taarifa zaidi za kiintelijensia zinasema, Makamu wa Rais aliyetimuliwa, Emmerson Mnangagwa, amekuwa akiandaa mpango wa uongozi baada ya Mugabe kuondoka madarakani akishirikiana na jeshi pamoja na upinzani kwa zaidi ya mwaka sasa.
Wakati huo huo, kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC, Morgan, Tsvangirai, ambaye amekuwa akipatiwa matibabu ya Saratani nchini Afrika Kusini na Uingereza amerejea Zimbabwe jana.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!