Thursday 16 November 2017

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA HAMAD NDIKUMANA

Wachezaji wa timu ya Rayon Sports Ismailla Diarra (kushoto) na Tidiane Kone (kulia),wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Hamadi Ndikumana Katauti kutoka nyumbani kwake Nyakabanda kwenda katika Msikiti Qaddafi uliopo Nyamirambo, Rwanda na baadaye walifanya mazishi jana jioni.

Baba mzazi wa Ndikumana baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa mwanae, Ndikumana akitokea burundi.Mama mzazi wa Ndikumana akisadiwa amebebwa baada ya kufika Nyumbani kwa mwanae Rwanda akitokea Burundi.Majirani wakiwa wanalia.Watoto wakiwa barabarani kuaga mwili wa Ndikumana wakati ukipelekwa katika Msikiti wa Qaddafi uliopo Nyamirambo, Rwanda.…Safari ya Kupeleka mwili wa marehemu msikitini ikiendelea.Ndugu wa Ndikumana akilia kwa uchungu.Baadhi ya waombolezaji wakiwa barabarani wakati wa kusindikiza mwili wa marehemu
        
Mwili wa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Hamadi Ndikumana Katauti (39) amezikwa jana kufuatia kufariki nyumbani kwake usiku wa kuamkia juzi, nchini Rwanda katika makaburi yaliokuwepo kwenye mji wa Nyamirambo, Rwanda.
Ndikumana ambaye alikuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irine Owoya amezikwa na mamia ya wadau wa soka nchini humo wakiwemo mashabiki wa klabu ya Rayon Sport ambayo alikuwa akifanyia kazi kama kocha msaidizi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!