Friday, 27 October 2017

Hadithi


MKONO WENYE DAMU YA MWANAE
(story fupi yenye funzo)
Ilikuwa ni siku ya Jumamosi mida ya mchana Mama Marry alikuwa amekaa sebureni na mwanae Marry.Alikuwa akiandika ripoti mbalimbali za ofisini ambazo hakumalizia siku ya ijumaa ili ikifika jumatatu siku ya kwenda kazini angalau awe amepunguza mzigo.


Wakati huo pia mwanae aliejulikana kwa Marry aliekuwa akisoma chekechea alimuona mama yake akiandika hivyo nae alitamani awe anaandika.Aliuendea mkoba wake uliokuwa na madaftari yake ya shule na kukaa sebureni pale mezani pamoja na mama yake.Wakati mama yake anaandika mambo yake ya ofisini Marry nae aliekuwa chekechea alichukua daftari zake na penseli na kuanza kuandika alphabet walizokuwa wakiimbishwa kila siku na mwalimu wao.Pia alikuwa ameshaanza kujua kuandika maneno kama vile "BABA","MAMA","DADA" na "KAKA".Alikuwa pia akiyaandika katika daftari lake lile la shule.
Ghafla Marry aliacha kuandika na kuanza kumshangaa mama yake vile anavyoandika.Mshangao huu ulisababishwa baada tu ya mama yake kuacha kuandikia kutumia biki na badala yake alichukua "Marker Pen" ili kuandika kichwa cha habari ambacho alitaka kiwe na maandishi makubwa hivyo alitumia Marker Pen yenye kutoa wino mwingi wenye kuonekana.
Marry alibaki akiishangaa ila Marker pen kwa jinsi inavyotoa wino wa rangi,hakuwahi kuiona na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza hivyo alivutiwa nayo.Alitamani na yeye atumie kuandikia angalau kwenye daftari lake kama mama yake anavyofanya.
Aliishangaa Biki ile kwa muda baadae uvumilivu ulimshinda akaamua amuombe mama yake angalau na yeye aitumie kuandika.Umri wake ulikuwa bado mdogo hivyo hata kuongea bado alikuwa hawezi kutamka maneno vizuri hivyo alisema"Mama Aomba na mimi hiyo".Mama yake akiwa bize na shughuri za ofisini alimjibu kwa mkato tu"Tumia kwanza hiyo".Alimaanisha kuwa aendelee kutumia penseli yake.
Marry alibaki akiiangalia pen ile ya mama yake kwa muda na hatimae alikata tamaa ya kuipata na akaamua aendelee tu kutumia Penseli yake kuandika Alphabet zake.
Baada ya kuandika kwa muda mrefu, Mama Marry alikuwa ametenga mboga jikoni na walikuwa bado hawajala mchana huo yeye na mwanae toka wanywe chai asubuhi.Alifunga vitabu vyake vizuri na kuviacha pale mezani kisha akanyanyuka na kuelekea jikoni kwa ajili ya kuendelea na upishi.Vitu vyake vyote aliviacha mezani zikiwemo zile biki aina ya Marker Pen pamoja na simu yake ya gharama sana aina ya Samsang S5 ambayo inauzwa si chini ya laki 5 pamoja na kile kitabu ambacho alikitumia kuandikia mambo ya ofisini.Mezani pale alimuacha Marry akiendelea na mambo yake ya chekechea
Alielekea jikoni kupika ili wale na hata mumewe atakapoludi pia akute chakula tayari.Ghafla akiwa anaendelea kupika jikoni mama Marry alisikia mlio wa kama siku yake imedondoka chini na kama vile sauti ya kioo kuvunjika.Akiwa jikoni aliita kwa hasira"We Marry wewe".Upesi upesi alitoka jikoni na kuelekea sebureni,Alimkuta Marry katoka pale mezani huku akitetemeka na akiwa ameshikilia ila Marker Pen ya mama yake ambayo alikuwa anaitamani mda mlefu sana kuitumia ili aandike alikuwa akitetemeka baada ya kugundua kuwa ameangusha simu ya mama yake,Mama alifika pale sebureni na kukuta meza yote imejaa maandishi ya marker Pen mpaka juu ya kitabu chake cha ofisini.Alipotazama chini aliona simu yake imeangushwa na tayari kioo kimevunjika.
Kwa hasira alimfuata Marry ambae wakati huo alikuwa ametambua kosa alilolifanya hivyo alikuwa ametoka mezani na kusogea mbali na meza,alikuwa ameelekea usawa wa kabati la sebureni mle.
Mama Marry kwa hasira na jazba baada ya kuona simu yake imevunjwa na faili lake la kazini limechafuriwa alinyanyua kibao kizito sana na kumpiga mwanae marry aliekuwa bado mdogo kabisa.Kibao kilikuwa cha kupigwa mtu mzima na si mtoto yule ambae bado mdogo kabisa.Nguvu ya kibao kile ilimpelekea Marry kujigonga kichwa chake kwenye mbao ngumu ya kabati iliyokuwepo karibu nae.Mama Marry huku akiwa amejaa jazba alimshuhudia mwanae badala ya kulia bali mwili wake na macho yake yalianza kuishiwa nguvu na hatimae kudondoka chini.Pale pale Jazba ya mama Marry iligeuka kuwa presha na uchungu kwa mwanae,Alianza kutetemeka huku akimtikisa mwanae na kumuita"Marry...Marry" lakini ilikuwa kimya.
Haraka haraka Mama marry huku akiwa kachanganyikiwa juu ya hali ya mwanae alimchukua na kumpakia kwenye gari ili ampeleke hospitali.
Aliendesha gari huku analia na akijuta kwanini ameyafanya yale kwa mwanae,kwanini amethamini mali na badala ya kumthamini mwanae.
Akiwa anaendesha gari aligundua kuwa mkononi mwake kuna damu ilikuwa imeganda,Pale pale alimgeukia mwanae Marry aliekuwa bado amefumba macho na kugundua kuwa baada ya kumchapa kibao damu ilimtoka puani Marry na kuruka hasa baada ya kujigonga kwenye mbao ya kabati na ndio hiyo nyingine ilimlukia mkononi.Mama Marry akiwa anaendesha gari kuelekea hospitalini alijikuta anaanza kulia kwa kwikwi huku akiwa na mashaka ya kumpoteza mwane
Alifika hospitalini akiwa kama kachanganyikiwa na kumbeba mwanae Marry moja kwa moja mpaka ndani ya hospitali,Wahudumu walimchukua mtoto Marry kwa ajili ya vipimo,Muda huo mama Marry nguo yake ilikuwa tayari imejaa machozi akimlilia mwane huyo.Aliona ni kama vipimo vinachelewa ili kujua hali ya mwanae.
Baada ya muda kidogo docta alieenda kuchukua vipimo alilejea na majibu,Mama Marry aliambiwa"Pole sana Mwanao hatuponae tena duniani vipimo vinaonesha ni kama amepata ajari mbaya sana sehemu ya kichwa iliyopelekea damu kuchanganyikana na ubongo hivyo kupoteza maisha yake."
Mama Marry aliposikia taarifa hiyo kabla hajaongea chochote alizimia.
Alikuja kuzinduka mida ya jioni akiwa nyumbani,hii ni baada ya moja ya wahudumu wa pale hospitali kumfahamu kisha kumpa taarifa mumewe kilichotokea.
Mama Marry hakutaka kuongea na mtu hata mmoja licha ya baadhi ya majirani kuwa tayari wameshaanza kukusanyika kwa ajiri ya kutenga msiba.Alinyanyuka na taratibu aliisogelea meza na kuanza kuiangalia,Meza ilikuwa imejaa maandishi ya Marry kila sehemu,Marry alikuwa amechafua meza ile kwa kujifunza kuandika maneno"BABA","MAMA" kila sehemu.
Mama Marry huku akijikuta anaanza kulia tena aliiokota simu yake pale chini iliyokuwa na rangi nyeupe na tayari kioo kilikuwa kimevunjika,aliigeuza kwa nyuma na kukuta pia Marry alikuwa ameiandika simu ile kwa nyuma kwa Marker Pen ile ya blue neno "MAMA" ila wakati anaiandika kwa bahati mbaya simu iliteleza pale mezani na kuanguka.
Mama Marry alizidi kulia zaidi kwa uchungu na kujutia kwanini alithamini sana mali kuliko Elimu ya Mwanae.
* * * * * * * MWISHO * * * * * * *
.....Katika maisha yetu tunayoishi wengi wetu tumejikuta tunathamini sana mali kuliko hata watoto wetu tuliowazaa,tumekuwa tukizipamba vizuri angali watoto wetu tukiwaacha uchi,Tumekuwa taraalamu sana wa kuweka SCREEN PROTECTOR NA COVER nzuri za bei katika simu zetu wakati huo kaptula na suruali wanazovaa watoto wetu zinavilaka na zingine zimetoboka,Kumbuka mali hiyo unayoijali lao ina muda wake wa ku expire na kufa kabisa,lakini mtoto unaemuacha hovyo leo na kutokumjali kama gari lako,au simu yako au nyumba yako kesho na kesho kutwa unategemea atakuwaje,thamini sana mtoto wako kwa sababu yeye hana mda wa ku expire na pia ni msaada mkubwa sana katika uzee wako kuliko hata mali uliyonayo leo ambayo haina uwezo hata wa kudumu miaka 20.
ASANTENI.
Mtunzi na Mwandishi
MARTIN B. MSAFIRI
CONT:0755278579

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!