Monday, 23 October 2017

DAKTARI: MWILI WA KANUMBA ULIKATWAKATWA VIPANDE


DAR ES SALAAM, TANZANIA
Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo imeambiwa kuwa mwili wa marehemu Steven Kanumba ulikatwa vipande vipande na kupelekwa kwa mkemia kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


Madai hayo yametolewa na Daktari Bingwa wa vifo vyenye utata na  magonjwa mbalimbali ya binadamu Innocent Mosha wakati akitoa ushahidi mbele ya Jaji wa Mahakama hiyo Sam Rumanyika.


Daktari huyo amedai vipande vilivyopelekwa kwa mkemia ni pamoja na kipande cha utumbo, chakula kilichomo, kipande cha ini, figo, mkojo, damu, majimaji kwenye jicho na kucha.

Akiongozwa na  wakili wa serikali Faraja George shahidi huyo amedai Aprili 9, 1012 akiwa kazini kwake katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokea amri halali ya polisi ikimwamuru kufanya uchunguzi wa mwili wa Kanumba uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Dakatari huyo bingwa amedai kuwa wakati wa uchunguzi huo walikuwa na mashahidi wawili walioenda kuangalia kama ana majeraha ya nje ya mwili.

Amedai kuwa kucha za vidole za marehemu Kanumba zilionekana kuwa na rangi ya bluu, pia walipofungua viungo vya ndani vya mwili wa marehemu kwenye sehemu ya kisogo kulikuwa na mvilio wa damu aidha baada ya kufungua fuvu la kichwa ubongo ulikuwa umevimba.

Daktari huyo bingwa aliendelea kudai kuwa kwenye mishipa midogo inayosambaza damu iliyokuwemo ilivia damu na sehemu ya chini ya ubongo kulikuwa na mkandamizo wa damu.

Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa alifungua mapafu, moyo, figo, maini, tumbo na mifumo mingine ya mwili haikuwa na tatizo lolote.

Alidai kwamba katika ripoti yake aliyoandaa kwenda kwa mkemia, ilionyesha kuwa ana tatizo kwenye mfumo wa upumuaji ambapo ulishindwa kufanya kazi kutokana na majeraha kwenye ubongo.

"Hakuna majeraha kwa nje lakini mapafu yalijaa damu ambapo tulikata kucha kufanya vinasaba, tulichukua majimaji ya kwenye jicho kuangalia kiasi cha pombe na suari kwenye mwili", alidai.

Pia alidai kuwa pombe haiwezi kusababisha matatizo hayo moja kwa moja badala yake mabadiliko ya tabia yanayotokana na unywaji ndiyo yanaweza kuchangia.

Alipoulizwa swali wakili wa utetezi Peter Kibatala shahidi alisema hatambui kama Seth Bosco alikuwepo wakati wa uchunguzi kwa sababu sio lazima mtu kuwepo mwanzo hadi mwisho.

Alieleza kuwa hafahamu kiwango cha pombe na  kama alijinyonga kwa sababu ya pombe na kwamba hawakuchukua sampuli ya ubongo




















Msanii wa Bongo Movie Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa na wazazi wake wakati wa kesi yake dhidi ya kifo cha kanumba, leo.






















Msanii wa Bongo Movie Elizabeth Michael 'Lulu' akipitia maelezo aliyotoa alipokamatwa na Polisi baada ya kifo cha Kanumba, alipokuwa Mahakama Kuu, leo












































Msanii wa Bongo Movie Elizabeth Michael 'Lulu' akitoka Mahakamani baada ya kusikiliza shahidi aliyefanyia uchunguzi mwili wa Kanumba

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!