Saturday, 2 September 2017

Wafungwa, JKT kujenga nyumba 402 za walimu Dar


UJENZI wa ofi si za walimu 402 katika Mkoa wa Dar es Salaam, unatarajiwa kuanza rasmi Septemba 5, mwaka huu na utafanywa na vijana 300 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na wafungwa kutoka Jeshi la Magereza.


Hayo yamesemwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitambulisha Kamati ya Ujenzi wa Ofi si hizo kwa shule za msingi na sekondari. Kamati ya ujenzi wa ofi si za walimu itaongozwa na Mwenyekiti, Kanali Charles Mbughe kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makamu Mwenyekiti ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, Solomoni Urio kutoka Jeshi la Magereza, Katibu wa Kamati ni Ofi sa Elimu wa Mkoa Hamis Lissu, Katibu Msaidizi ni SACP Juma Hamis kutoka Jeshi la Polisi pamoja na wajumbe.
Makonda alisema ujenzi wa ofi si hizo, unafanyika baada ya kuzungumza na walimu ambao walibainisha kuwa kero kubwa katika kazi zao ni uhaba wa ofi si, hali inayopunguza morali wa kazi na kuleta matokeo mabaya. Alitaka wananchi na wadau, kutoa michango kufanikisha ujenzi huo. Alisema ofi si hizo zitajengwa chini ya vyombo vya ulinzi na usalama kutoka JKT, ambao tayari wametoa vijana 300 kwa ajili ya ujenzi wakishirikiana na Jeshi la Magereza, ambalo litatoa wafungwa ambao watasaidia kufyatua matofali.
Aidha Makonda aliwaomba wadau na wananchi kuchangia fedha na vifaa ikiwemo mabati, nondo, saruji, kokoto, mchanga, mbao na nguvu kazi ya watu ili kuwafanya walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri. Alisema kuwa wananchi wanaotaka kuchangia wanaweza kuchangia fedha kupitia Akaunti ya CRDB Namba 0150296180200 au kuwasilisha michango yao Ofi si ya Mkuu wa Mkoa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!