Mkali wa muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahimu Musa ‘Roma Mkatoriki, baada ya juzi kuibukia Shule ya Mchikichini iliyopo Mbagala Rangi Tatu, jana Ijumaa Juni 16 mkali huyo alifuturu na watoto yatima katika kituo cha Dira kilichopo mitaa ya kwa Mzungu Mbagala Jijini Dar.
Akizungumza na Global TV Online, Roma alisema aumuzi wa kwenda kufuturu na watoto yatima katika kituo hicho umekuja baada ya kuona ana kila sababu ya Kuungana na watoto yatima na kuwatia moyo katika maisha yao kuelekea kilele ya siku ya watoto duniani.
“Tuko katika maadhimisho ya siku ya watoto ulimwenguni, kimisingi nimefurahi kufuturu pamoja na watoto yatima wa kituo hiki.
“Lakini pia nimepata nafasi ya kuwatia moyo na kuzungumza nao mambo mbalimbli kuhusu maisha, watoto pia wamefurahi kuniona na wamepata fursa ya kuniuliza mambo mengi.
“Nimeambiwa kuna changamoto nyingi hapa kituoni, nimewahidi nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha changamoto zile tunazimaliza siku za hivi karibuni kwa kushirikiana na wasanii wenzangu wa hapa nchini” alisema rapa huyo ambaye aliandamana na mkewe katika hafla hiyo.
Naye mlezi wa kituo hicho Bi Edis Isdori alimshukuru msanii huyo kwa moyo wake kwa kuwateembelea katika kituo chao na kutoa wito kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kurudi katika jamii zao na kushiriki katika mambo mbalimbali.
“Namshukuru Roma mkatoriki kwa kuja na kutufuturisha pamoja na watoto, ukweli ni kwamba watoto wamefurahi na wamefarijika sana.
“Nnitoe wito kwa wasanii wengine wawe na moyo kama wa msanii huyu kwa kuja kwenye jamii na kushiriki pamoja katika mambo mbalimbali.”
STORI: Na Ally Katalambula
No comments:
Post a Comment