Sunday 28 May 2017

Watatu wafariki katika bwawa baada mtumbwi kuzama

Image may contain: tree, outdoor, nature and water
RUFIJI, PWANI: Watu watatu wamefariki na mmoja amenusurika baada ya Mtumbwi waliokuwa wakiutumia kuvukia kuzama ktk Bwawa la Umwe.


Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo, Ofisa Tarafa ya Ikwiriri, Suleimani Mpangile aliwataja marehemu hao kuwa ni Sijali Abdallah (14), Zuberi Penya (11) wakazi wa Umwe Ikwiriri na Salehe Saidi (31) mkazi wa Dar es Salaam. 

Mpangile pia alimtaja aliyenusulika kifo kuwa ni Musa Mkamba ambaye alikuwa akiwavusha marehemu hao. 

Alisema chanzo cha vifo hivyo ni mtumbwi waliokuwa wakivukia kujaa maji na kuzama jana Jumamosi saa 3 asubuhi katika bwawa hilo la Umwe.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!