Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi ya kukutwa na bhangi inayomkabili msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Isaack Sepetu (28) na wenzake wawili akiwemo mfanyakazi wake wa ndani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umekamilika.
Wakili wa Serikali, Onolina Moshi amesema hay leo (Jumanne) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Hivyo aliomba kesi hiyo iahirishwe na ipangiwe tarehe kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH).
Kutokana na ombi hilo kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni Mosi,2017 kwa PH.
Wema aliwakilishwa mahakamani hapo na Wakili Tundu Lissu.
Mbali na Wema wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima wote wanatetewa na wakili Kibatala na Hekima Mwesigwa.
Inadaiwa kuwa Wema ambaye ni mshindi wa taji ya Urembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 , Februari 4 mwaka 2017, nyumbani kwake, Kunduchi Ununio, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa na bhangi, msokoto mmoja na vipande viwili vya bhangi.
MWANANCHI:
MWANANCHI:
No comments:
Post a Comment