Friday 26 May 2017

MTOTO ALIYEWAOKOA WATOTO WENZIE ASIMULIA MKASA


"Naitwa Tisekwa Gamungu nipo darasa la Tano na nina miaka 16. Ilikuwa jumatatu tumetoka shuleni na wenzangu, tulifika sehemu ya kupanda Boti tulifanikiwa kupanda boti na wenzangu lakini tulivyofika katikati boti zetu zilizama ikabidi niogelee na wenzangu ili kuweza kutoka nchi kavu lakini wenzangu wengine walishindwa. 



Hivyo ilinibidi niingi kuwaokoa wenzangu kwani moyo ulikuwa unaniuma kuwaacha wenzangu wazame wakati nina uwezo wa kuwasaidia. Nilifanikiwa kuwaokoa wenzangu 9. Wakati naendelea kuwaokoa, wenzangu 3 walichoka sana kwaiyo walizama. Nikajitahidi kuwatafuta lakini sikuwaona." 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!