Monday 22 May 2017

MOHAMED ABDALLAH AMEFARIKI DUNIA HUKO ZANZIBAR WAKATI AKIJARIBU KUMUOKOA PAULO ALIYEKUWA AKIZAMA KATIKA MAJI.

Image may contain: one or more people and outdoor
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mohammed Abdalla ambaye ni Dereva wa Daladala ya Chuo Kikuu amefariki Dunia baada ya kujaribu kumuokoa Dereva wa Bodaboda aliyejulikana kwa jina la Paulo ambaye alikua anazama katika eneo la Fuoni Kibonde Mzungu.


Wakati akimsaidia kumuokoa ndipo inasadikiwa aliteleza na kupelekea maji kumzidi na kumsukuma na hadi anaokolewa alikuwa tayari ameshafariki dunia.
Ni siku 10 tu zimepita tangu limetokea tukio kama hilo katika eneo hilo la Fuoni Kibonde Mzungu ambapo May 12 Askari polisi Abasi Anasi alipoteza maisha yake hapohapo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Chanzo : Zanzibar24

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!