Sunday, 21 May 2017

Leo ni siku ya Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba Mei 21, 1996




MV-Bukoba2

Meli ya MV Bukoba ikiwa Ziwa Victoria wakati ilipokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kuzama.
KIUKWELI tarehe kama ya leo miaka 21 iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya Watanzania na Ulimwenguni kote, kwani usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, meli ya MV Victoria ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu.


MV-BukobaMeli ya Mv Bukoba ikiwa inazama.
Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.
image_1Mnara wa Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba uliopo Makaburi ya marehemu waliotokana na ajali hiyo, Igoma - Mwanza.
Hakika Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la Tanzania liligubikwa na Msiba Mkubwa ambapo kila mmoja kwa nanma yake aliguswa na Msiba huo ambao uliyagharimu Maisha ya Mamia ya Wapendwa Wetu, baada ya Meli ya MV.Bukoba Kuzama hatua chache kabla ya kutia Nanga Mkoani Mwanza ikitokea
Mkoani Kagera.
Meli ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilizama katika Maji ya Ziwa Victoria Mkoani Mwanza yapata umbali wa kilomita zipatazo 30 kutoka ufukweni mwa maji na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika Meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17. Jambo la butwaa hapa ni Idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa ukilinganisha na Uwezo uwezo wa Meli hiyo wa kubeba abiria 430).
makaburi ya mv bukoba (5)Makaburi ya waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Bukoba yaliyopo, Igoma - Mwanza.
Pengine tumezoea kuita kwamba Mei 21 Watanzania tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzama kwa Meli hiyo ambayo iliigeuza taswira ya Mji wa Mwanza, kwani kwa waliokuwa Mwanza Mwaka huo walipigwa na Butwaa baada ya Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ambao mara nyingi hutumika kwa
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
Wakati leo tunakumbuka tukio hili ambalo limeacha simanzi mioyoni mwetu, hebu tujiulize kwa pamoja; Kama ilivyo imani ya watalaamu wa masuala ya usafiri kwamba Usafiri wa Majini ndio usafiri
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.


CRD: 2Jiachie blog

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!