Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akizungumza jambo na walimu wa viwanja vya JK Youth Park mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuifunda timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) akiwa kwenye ziara ya siku tatu nchini.
Katika siku yake ya tatu (leo) nchini gwiji huyo wa soka atashuhudia fainali ya timu tatu kutoka nchini za Tanzania, Uganda na Kenya ambao watapambana vikali kuwania kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield mjini Liverpool nchini Uingereza. Barnes amesistiza muhimu wa kuwafunda vijana wadogo wakiwa katika umri mdogo kabisa kama njia bora ya kuwaandaa kuwa wachezaji bora siku za usoni na kuwa tegemeo katika nchini yao. Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Bi Juanita Mramba amesema kwamba Azania Group of Companies kutoka Tanzania, Capital Fm-Kenya na Coca Cola ya Uganda watamenyana vikali kwenye fainali hizo kesho kwenye viwanja vya Jk Youth Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. “Tumeweza kumleta John Barnes kushiriki kwenye mazoezi ya vijana chini ya miaka 15 kwa ajili ya kuwaanda kwenye mashindano ya AFCON ya vijana mwakani, lakini pia amekuja kwa ajili ya tukio la benki hiyo kutimiza miaka 100 tangu kuanza shughuli zake mwaka 1917 za kibenki nchini,” amesema Mramba
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza machache na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kabla ya kuelekea uwanjani kuwafunda kwa vitendo katika viwanja vya JK Youth Park, Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kwamba takribani timu 32 zilishiriki kwenye mashindano ya awali ya kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika fainali zitakazofanyika kesho na timu mbili kutoka Uganda na Kenya.
Mramba alifafanua kwamba gwiji huyo wa soka aliyetamba miaka ya 1990 atakuwa nchini kwa siku tatu na kushiriki kwenye program ya kuwafundisha vijana wa umri chini ya miaka 15 kuwapa mbinu za soka tangu wakiwa vijana wadogo.
Kwa upande wake, Msemaji wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Bw Alfred Lucas amesema kwamba hii ni fursa adimu kwa vijana kupata nafasi ya kufundishwa soka na mmoja wa magwiji wa soka wa dunia.
“hii ni nafasi yao muhimu sana katika kujifunza mambo ya soka na kupanua uelewa wao kuhusu mpira wa miguu wakiwa bado vijana wadogo kabisa maana ni mastaa wa taifa wa baadaye,”
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes (kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (wa kwanza kushoto) wakionyeshana jambo kwenye viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Aidha, kocha wa timu ya Serengeti Boys, Kim Poulsen aliwashukuru benki ya Standard Chartered kwa kufanikisha ujio wa gwiji hilo la soka kuja kushiriki kwenye mazoezi na kutoa mchango wa mafunzo kwa vijana wake.
Aliongeza kwamba ni muhimu kwa wadau wengine wa michezo kuiga mfano wa benki hiyo na kuweza kuwaleta magwiji wa soka duniani kama chachu ya maendeleo ya soka kwa nchini zinazoendelea kama Tanzania.
Gwiji hilo la soka kutoka klabu ya Liverpool anatarajiwa kuondoka leo jioni baada ya fainali hizo kwenye viwanja vya JK Youth Park mjini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati pia akimtambulisha gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpoool John Barnes (hayupo) wakati wa kliniki fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) iliyoendeshwa na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kuwawekea mazingira na miundombinu ya kutosha watoto ili kuweza kuinua maendeleo ya soka nchini.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwenye soka la watoto chini ya umri wa miaka 15 kama njia bora ya kukuza vipaji nchini wakati wa kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa Soka wa timu ya Liverpool, John Barnes katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa John Barnes na umuhimu wa kuinua vipaji kwa watoto chini ya miaka 15.
Pichani juu na chini ni John Barnes akiwapa mbinu mbalimbali wakati wa mazoezi kwa watoto chini ya umri wa miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kupata fursa ya kuwepo nchini kushuhudia fainali za mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield katika kuadhimisha miaka 100 tangu benki ya hiyo kuanzishwa nchini yatakayofanyika leo katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) wakitoana jasho baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa soka wa timu ya Liverpool, John Barnes (hayupo pichani) katika viwanja vya JK Youth Park, jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen wakiwatazama timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji huyo jana katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akibadilishana uzoefu na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen (kushoto) wakati wa kliniki fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa wateja wa benki ya Standard Chartered waliopata nafasi ya kukutana na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park.
No comments:
Post a Comment