Monday 20 February 2017

Toka kwa Dina Marios!


Maisha yana purukushani nyingi sana ambazo zinaweza kukupa msongo wa mawazo.Maisha magumu,magonjwa,kazi kubwa mshahara mdogo,mara kodi ya nyumba imepanda,ile frame kodi imeongezwa,kazini watu wanakupiga vita,umetelekezwa na mwanaume kakuacha na mtoto yaaani vurugu ni nyingi sana wewe mwenyewe unajau.


Ambazo huiweka nafsi na roho yako juu juu huna raha wala amani.
Vyovyote iwavyo Jitahidi kutafuta amani ya moyo.Amani ya moyo hailetwi na mtu usimtegemee mtu kukupa amani ya moyo.Tena mtu anaweza kukudisapoint.
Amani ya moyo hailetwi na vitu eti labda huo mshahara ukipanda kazini utakuwa na raha na amani,ukipata pesa,ukijenga nyumba hakuna kitu kama hicho.Always always changamoto zipo na ndio dunia inavyokwenda.Kubwa tafuta amani ya moyo....kujikubali,kukubali situation uliyopo,kukubali kuna mambo huwezi kubadilisha na kuyaacha kama yalivyo,kulet go of the past,na zaidi kuwa strong kiimani.
Upe moyo wako amani...usiuchoshe..tafuta amani ya moyo wako.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!